Chombo cha anga ya juu cha Kenya kilichotengenezwa na Chuo cha Machakos chatarajiwa kurushwa angani na roketi ya China
2021-08-31 14:50:12| cri

Chombo cha anga ya juu cha Kenya kilichotengenezwa na Chuo cha Machakos chatarajiwa kurushwa angani na roketi ya China_fororder_timg (2)

Kipindi cha Daraja kinachokujia kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) kinakufahanmisha mambo mbalimbali kuhusu uhusiano, ushirikiano na mawasiliano kati ya China na Afrika. Katika kipindi cha leo, licha ya habari wiki hii zilizohusisha China pamoja na nchi za Afrika, tutakuwa na ripoti itakayohusu jinsi kampuni za China zinavyosaidia nchi za Afrika katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria, na pia tutakuwa na mahojiano kutoka studio ya CMG Idhaa ya Kiswahili mjini Nairobi kuhusu chombo cha anga ya juu cha Kenya kilichotengenezwa na Chuo cha Machakos ambacho kinatarajiwa kurushwa angani hivi karibuni na roketi ya China.