MINUSMA: Raia wasiopungua 527 wamekuwa wahanga wa migogoro nchini Mali katika robo ya pili ya mwaka 2021
2021-08-31 09:37:43| cri

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Tume ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini Mali (MINUSMA), raia wasiopungua 527 wamekuwa wahanga wa vurugu za ukiukaji wa haki za binadamu nchini Mali katika robo ya pili ya mwaka 2021, wakiwa wameuawa, kujeruhiwa, kutekwa nyara au kutoweka, ambao wameongezeka kwa asilimia 25 ikilinganishwa na robo ya kwanza ya mwaka huu.

Asilimia 20 ya vurugu hizo nchini Mali zimesababishwa na wapiganaji wenyeji na vikundi vya kujilinda huku operesheni mbalimbali za majeshi ya kimataifa na Jeshi la Mali pia zimesababisha ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya wenyeji.

Habari nyingine zinasema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu wiki hii lilipitisha uamuzi wa kurefusha vikwazo dhidi ya Mali kwa mwaka mmoja hadi tarehe 31, Agosti mwaka kesho. Vikwazo vilivyorefushwa ni pamoja na zuio la kusafiri na kuzuiwa kwa mali dhidi ya watu binafsi na mashirika yaliyotambuliwa na Kamati ya Vikwazo kwa kukiuka haki za binadamu nchini humo.