Msemo huu ulianza kujulikana tangu miaka 1,500 iliyopita hapa China, ukimaanisha kwamba hatupaswi kuogopa taabu, na lengo lolote lile tukilivalia njuga na kujitahidi kulitekeleza, basi iko siku tutalitimiza. Waswahili pia wana msemo unaolingana na huu usemao“haba na haba hujaza kibaba”, jambo lolote lile ukilianza taratibu mwisho utafanikiwa.