Msumbiji yafanya maonesho ya kimataifa ya mwaka kuhimiza biashara na uwekezaji
2021-08-31 09:06:34| CRI

Awamu ya 56 ya Maonesho ya Kimataifa ya Maputo (FACIM), ambayo ni maonesho makubwa zaidi ya kibiashara nchini Msumbiji, yalifunguliwa Jumatatu katika mkoa wa kusini wa Maputo.

Akiongea kwenye sherehe ya ufunguzi wa maonesho hayo ya kila mwaka, rais Filipe Nyusi wa Msumbiji alisema maonesho hayo yanapaswa kusaidia kuvutia uwekezaji na kuziweka kampuni za kitaifa kwenye viwango vya kimataifa.

Rais Nyusi amesema serikali yake itaendelea kuondoa vizuizi vya urasimu, ili kuyafanya mazingira ya biashara yawe na mvuto, ushindani, yenye kutabirika, na kupunguza sintofahamu kwa wawekezaji.