Baraza la usalama la UM lapitisha azimio kuhusu Afghanistan baada ya Taliban kuingia madarakani
2021-08-31 09:15:18| CRI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio kuhusu Afghanistan baada ya Taliban kuingia madarakani, likilenga mapambano dhidi ya ugaidi na kutoa misaada ya kibinadamu.

Azimio nambari 2593 linataka ardhi ya Afghanistan isitumike kutishia au kuishambulia nchi yoyote, au kuwahifadhi na kuwapa mafunzo magaidi, au kupanga na kufadhili vitendo vya kigaidi. Azimio hilo pia limesisitiza umuhimu wa kupambana na ugaidi nchini Afghanistan kuwakumbusha Taliban kuhusu ahadi zao.

Azimio hilo pia limekumbusha taarifa ya Taliban iliyotolewa ijumaa, inayosema watu wa Afghanistan wataruhusiwa kusafiri nje ya nchi, wanaweza kutoka nje ya Afghanistan wakati wowote wanaotaka, wanaweza kutoka nje ya nchi kwa njia yoyote wanayotaka iwe kwa ndege au barabara, ikiwa ni pamoja na uwanja wa ndege wa Kabul, na hakuna atakayewazuia kusafiri.