Kamanda wa jeshi la Marekani asema uondoaji wa jeshi la Marekani umekalimika
2021-08-31 09:14:30| CRI

Kamanda wa jeshi la Marekani asema uondoaji wa jeshi la Marekani umekalimika

Kamanda wa jeshi la Marekani amesema uondoaji wa jeshi la Marekani kutoka Afghanistan umekamilika, na kukomesha miaka 20 ya uvamizi ulioongozwa na jeshi la Marekani nchini humo.

Kamanda wa Kamandi Kuu ya jeshi la Marekani Kenneth McKenzie ametangaza kumalizika kwa kazi ya kuwaondoa raia wa Marekani, raia wa nchi ya tatu na waafghanistan walio hatarini. Amesema ndege ya mwisho kuwaondoa watu hao iliruka alfajiri ya jana kutoka uwanja wa ndege wa Hamid Karzai.

Hata hivyo amesema ubalozi wa Marekani utaendelea kuwa wazi kuhakikisha wamarekani na raia wa Afghanistan wanaotaka kuondoka waweze kuondoka. Amesema kwa sasa idadi ya wamarekani waliokwama nchini Afghanistan ni ndogo ambayo iko mamia.