Mawaziri wa Umoja wa Ulaya waapa kushirikiana na UM kwenye suala la Afghanistan kutokana na hofu ya uhamiaji haramu
2021-09-01 09:00:53| CRI

Mawaziri wa Umoja wa Ulaya waapa kushirikiana na UM kwenye suala la Afghanistan kutokana na hofu ya uhamiaji haramu_fororder_VCG111345954485

Maofisa waandamizi kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wameahidi kushirikiana na Umoja wa Mataifa kutuliza hali baada ya Taliban kudhibiti Afghanistan, wakiwahimiza Taliban kukata mahusiano na vitendo na ugaidi wa kimataifa.

Mawaziri wa Sheria na Mambo ya Ndani wa nchi za Umoja wa Ulaya wamesema kupitia taarifa kufuatia mkutano uliofanyika Brussels, kuwa Umoja huo na nchi wanachama wake 27 wanadhamiria kuchukua hatua za pamoja ili kuzuia kutokea kwa uhamiaji haramu usiodhibitiwa wa idadi kubwa ya watu kama ulivyotokea zamani, kwa njia ya kuandaa mwitikio wenye uratibu.

Maofisa hao wameahidi kuzisaidia nchi jirani za Afghanistan kuwapokea wakimbizi kutoka nchi hiyo, wakidai kuwa kazi hiyo itafanyika kwa msingi wa hiari huku wanawake na watoto wakipewa kipaumbele.