Rais Xi Jinping wa China atoa hotuba kwenye mkutano wa kilele wa biashara ya huduma duniani
2021-09-02 20:54:06| CRI

Rais Xi Jinping wa China atoa hotuba kwenye mkutano wa kilele wa biashara ya huduma duniani_fororder_2021090220405547359

Rais Xi Jinping wa China leo ametoa hotuba kwa njia ya video kwenye mkutano wa kilele wa biashara ya huduma wa Maonyesho ya biashara ya huduma ya kimataifa ya China ya mwaka 2021.

Rais Xi Jinping amesema, China inapenda kushirikiana na pande mbalimbali, kuendelea kufungua mlango na kufanya ushirikiano, kunufaishana,kufaidika kwa pamoja na fursa ya maendeleo ya biashara ya huduma, na kuhimiza ufufukaji na ongezeko la uchumi duniani.

Rais Xi ameongeza kuwa, China itaimarisha ujenzi wa kanuni katika sekta ya huduma, kuunga mkono Beijing na sehemu nyingine kutangulia kufanya majaribio na utekelezaji kuendana na kanuni za makubaliano ya biashara huria yenye kiwango cha juu, na kujenga eneo la kielelezo la biashara ya kidijitali. Aidha, China itaendelea kuunga mkono maendeleo ya makampuni madogo na yenye ukubwa wa kati, kupanua mageuzi ya “Bodi Tatu Mpya”, kuanzisha soko la hisa la Beijing, na kuanzisha jukwaa la kuhudumia makampuni madogo na yenye ukubwa wa kati.