Zaidi ya watumishi 40 wa afya wa Sudan Kusini wakamilisha mafunzo ya lugha ya kichina
2021-09-02 09:07:16| CRI

Zaidi ya watumishi 40 wa afya wa Sudan Kusini wamehitimu mafunzo ya miezi mitatu ya lugha ya kichina.

Kaimu mkurugenzi wa hospitali ya mafunzo ya Juba Bw. Alier Nyok amewapongeza watumishi hao ikiwa ni pamoja na madaktari, wauguzi na wakunga kwa kuhitimu mafunzo hayo, na kusema lugha hiyo itawasaidia kwenye mawasiliano kati yao na wenzao wa China. Amesema wachina wamepiga hatua moja zaidi kufanya uhusiano uwe rahisi.

Mafunzo hayo yalianza mwezi Juni yakiendeshwa na kikundi cha nane cha wahudumu wa afya kutoka China, kilichofika nchini Sudan Kusini mwezi Agosti mwaka jana kutoka mkoani Anhui.

Balozi wa China nchini Sudan Kusini Bw. Hua Ning amewapongeza watumishi wa Sudan Kusini na wahudumu wa afya kutoka China, kwa kukamilisha mafunzo hayo, na kusema anatarajia mafunzo hayo ya lugha yataimarisha mawasiliano ya watu na watu na hata uhusiano kati ya nchi hizo mbili.