Waziri wa mambo ya nje wa China afanya mkutano wa video na mjumbe wa rais wa Marekani anayeshughulikia suala la tabianchi
2021-09-02 09:21:00| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amefanya mkutano kwa njia ya video na mjumbe maalumu wa rais wa Marekani anayeshughulikia suala la tabianchi John Kerry ambaye yuko ziarani huko Tianjin kushiriki katika mazungumzo ya mabadiliko ya tabianchi kati ya China na Marekani.

Bw. Wang amesema China na Marekani zikiwa nchi kubwa duniani, ushirikiano ni chaguo pekee sahihi, ambao pia ni matarajio ya jumuiya ya kimataifa. Amesema China na Marekani zimewahi kufanya mazungumzo na ushirikiano wenye manufaa kwenye sekta za pande mbili na masuala muhimu ya kimataifa na ya kikanda ikiwemo mabadiliko ya tabianchi. Hali hiyo imetoa ishara muhimu kwamba pande mbili zinatakiwa kuheshimiana, kutafuta maslahi ya pamoja licha ya kuwepo tofauti kati yao, na kufanya ushirikiano wa kunufaishana.

Bw. Kerry amesema, ushirikiano kati ya Marekani na China ni muhimu katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Amesema Marekani inapenda kuheshimiana na China, kuimarisha mawasiliano na mazungumzo, ili kuhimiza utekelezaji wa makubaliano ya Paris.