Rais Xi awataka maofisa vijana kuimarisha utiifu na weledi kwenye majukumu muhimu
2021-09-02 09:07:47| CRI

Rais Xi awataka maofisa vijana kuimarisha utiifu na weledi kwenye majukumu muhimu_fororder_2021090120442384580

Rais Xi Jinping wa China ametoa mwito kwa maofisa vijana kuimarisha maadili yao, kuwa watiifu kwa chama, kutafuta ukweli kutoka kwenye mambo halisi, kubeba wajibu, kujitahidi kuwa uti wa mgongo wa jamii wakiaminiwa na chama na wananchi kutekeleza majukumu muhimu.

Rais Xi amesema hayo wakati akitoa hotuba kwenye ufunguzi wa mafunzo ya maofisa vijana na wenye umri wa kati yanayofanyika kwenye chuo cha kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China CPC. Pia amesema maofisa vijana wamezaliwa na kukulia katika zama nzuri, na kuwa wao ni sehemu muhimu ya chama na wananchi.

Pia amewakumbusha maofisa hao kutafuta heshima kwa kufanya kazi katika mazingira magumu ya maeneo ya mbali, na kusema mafanikio huwa hayapatikani bila jasho na uzoefu mkubwa.