Waziri mkuu wa Japan kuacha uchaguzi wa kiongozi wa LDP
2021-09-03 14:36:05| CRI

Waziri mkuu wa Japan kuacha uchaguzi wa kiongozi wa LDP_fororder_VCG111344053041

Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga amesema hatashiriki katika uchaguzi ujao wa kiongozi wa chama tawala cha Liberal Democratic Party (LDP). Hali ambayo inamaanisha kuwa ataacha kuendelea kuwa waziri mkuu wa Japan.

Suga jana alifanya mazungumzo na katibu mkuu wa LDP Toshihiro Nikai. Shirika la Habari la Japana Kyodo limechambua kuwa, watu kutoridhika na hatua za serikali za kukabiliana na janga la COVID-19 kunaweza kuwa sababu kuu ya Suga kuacha kushiriki kwenye uchaguzi.

LDP imepanga kuanza kampeni ya uchaguzi tarehe 17 na kufanya uchaguzi wake wa urais tarehe 29 mwezi huu.