Rais Xi Jinping ashiriki na kuhutubia sherehe ya ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Uchumi la nchi za Mashariki
2021-09-03 19:43:39| cri

Rais XI Jinping ashiriki na kuhutubia sherehe ya ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Uchumi la nchi za Mashariki_fororder_图像_2021-09-03_194316

Rais Xi Jinping wa China leo ameshirikina kuhutubia sherehe ya ufunguzi wa mkutano wa sita wa baraza la Uchumi wa Mashariki uliofanyika mjini Beijing kwa njia ya video, na kutoa mwito kwa nchi za Asia Kaskazini mashariki kuungana mikono ili kukabiliana na wakati mgumu na kupanga maendeleo ya pamoja.

Rais Xi amekumbusha kuwa leo ni siku ya kumbukumbu ya miaka 76 tangu China ipate ushindi katika vita dhidi ya uvamizi wa Japan na vita dhidi ya ufashisti duniani. Pia amekumbusha kuwa jumuiya ya kimataifa ni lazima itetee kwa nguvu matokeo ya ushindi ya vita ya pili ya dunia, ilinde ukweli wa historia, na ijitolee kutumia historia kama kioo ili kufungua siku nzuri zaidi za baadaye.

Rais Xi pia amesema mazingira ya sasa ya kimataifa yanapitia mabadiliko makubwa, janga la COVID-19 linaendelea kuleta changamoto za mara kwa mara, na uchumi wa dunia unakabiliwa na hali ngumu ya kufufuka. Ametoa wito kwa pande zote kuongeza juhudi za kuendeleza ushirikiano wa kunufaishana, kuimarisha ushirikiano kupitia pendekezo la "Ukanda mmoja, Njia moja"  na Jumuiya ya uchumi ya nchi za Ulaya na Asia, kuunga mkono maendeleo ya uvumbuzi wa uchumi wa kidijitali, kukabiliana kwa pamoja na mabadiliko ya tabia nchi duniani, na kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika kanda hiyo.