Thamani ya biashara kati ya China na Afrika yaongezeka kwa asilimia 40.5 kati ya Januari hadi Julai
2021-09-03 16:04:32| cri

Thamani ya biashara kati ya China na Afrika yaongezeka kwa asilimia 40.5 kati ya Januari hadi Julai_fororder_外贸集装箱

Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Biashara ya China zinaonesha kuwa, kati ya mwezi Januari hadi Julai mwaka huu, thamani ya biashara kati ya China na nchi za Afrika imefikia dola bilioni 139.1 za Kimarekani, na kuongezeka kwa asilimia 40.5 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hicho.

Naibu Waziri wa Biashara wa China Qian Kemin amesema katika miaka ya hivi karibuni, ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Afrika umeendelea kwa kiasi kikubwa. Haswa wakati wa kukabiliana na janga la COVID-19, pande hizo mbili zimeshikamana na kushirikiana bega kwa bega, na kuhimiza ushirikiano huo kuendelea kukua kwa haraka.