Ujinga wa kutojua kusoma na kuandika ni suala la kijamii kote duniani, ambao umezuia maendeleo ya jamii. Tarehe 17 Novemba mwaka 1965, Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa limeamua kuthibitisha tarehe 8 Septemba ya kila mwaka kuwa Siku ya Kimataifa ya Kufuta ujinga wa kutojua kusoma na kuandika, ili kuhamasisha nchi mbalimbali na mashirika husika ya kimataifa kupambana na hali hiyo, kuhimiza nchi mbalimbali kueneza elimu ya msingi, kuinua kiwango cha elimu ya msingi, ili watoto wanaofikia umri unaofaa wanaweza kwenda shuleni na kufikia kiwango cha kimsingi cha kusoma na kuandika, hatimaye kutimiza lengo la kuimarisha mawasiliano kati ya watu, kuondoa ubaguzi na kuhimiza uenezi wa utamaduni na maendeleo ya jamii.