Dozi milioni 30 za chanjo za COVID-19 za China kusafirishwa kwenda nchi kadhaa zinazoendelea
2021-09-03 09:41:06| CRI

Dozi milioni 30 za chanjo za COVID-19 za China kusafirishwa kwenda nchi kadhaa zinazoendelea_fororder_VCG111317406817

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin, amesema China siku zote inaunga mkono na kushiriki kwenye mpango wa usambazaji wa chanjo za COVID-19 COVAX, huku ikifanya juhudi kuhimiza upatikanaji wa chanjo katika nchi zinazoendelea. Hivi karibuni, dozi karibu milioni 30 za chanjo zitasafirishwa kwa nyakati tofauti kwenda Algeria, Cote d'Ivoire, Niger, Kyrgyzstan na Venezuela.

Bw. Wang amesema katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, baada ya kampuni za Sinopharm na Sinovac za China kupata idhini ya matumizi ya dharura ya Shirika la Afya Duniani WHO, kampuni husika zimehakikisha uzalishaji na kufanya mazungumzo kuhusu utoaji wa chanjo na Muungano wa Chanjo Duniani GAVI na kuorodheshwa kwenye ghala la manunuzi la COVAX mwezi wa Julai mwaka huu. Kwa mujibu wa makubaliano wa manunuzi yaliyosainiwa, kampuni hizo mbili zitatoa dozi milioni 110 za chanjo za COVID-19 kwa COVAX kabla ya mwisho wa Oktoba.