Rais Xi Jinping atoa hotuba kwa njia ya video kwenye Mkutano wa Kilele wa Biashara ya Huduma Duniani wa CIFTIS
2021-09-03 09:10:31| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana usiku alitoa hotuba kwa njia ya video kwenye Mkutano wa Kilele wa Biashara ya Huduma Duniani wa Maonesho ya Biashara ya Huduma ya Kimataifa ya China ya mwaka 2021 (CIFTIS).

Kwenye hotuba yake, Rais Xi Jinping amesema biashara ya huduma ikiwa ni sehemu muhimu ya biashara ya kimataifa na nyanja muhimu ya ushirikiano wa kiuchumi wa kimataifa, inachukua nafasi muhimu katika kujenga muundo mpya wa maendeleo. Amesema China inapenda kushirikiana na pande mbalimbali kwa njia ya wazi na ya kunufaishana, na kutumia kwa pamoja fursa za maendeleo kwenye biashara ya huduma, ili kuhimiza kwa pamoja ufufukaji na ukuaji wa uchumi wa dunia.

Maonesho ya Biashara ya Huduma ya Kimataifa ya China ya mwaka 2021 (CIFTIS) yanafanyika kuanzia tarehe 2 hadi tarehe 7 mwezi Septemba hapa Beijing, yakiwa na kaulimbinu “Dijitali Yafungua Mustakbali, Huduma Yahimiza Maendeleo”.