Kenya yapokea dozi 358,200 za chanjo ya COVID-19
2021-09-03 09:34:51| CRI

Wizara ya Afya ya Kenya jana ilipokea dozi 358,200 za chanjo ya COVID-19 ya AstraZeneca ili kuimarisha vita dhidi ya janga hilo nchini humo.

Waziri wa afya wa Kenya Bw. Mutahi Kagwe amesema chanjo iliyotolewa na serikali ya Canada itaiwezesha Kenya kutoa chanjo kwa watu milioni 10 kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Bw. Kagwe amesema Kenya imepokea zaidi ya dozi milioni 3.6 za chanjo ya COVID-19 na wizara ya afya ya Kenya inatekeleza kampeni thabiti, endelevu ya utoaji wa chanjo dhidi ya janga hilo na kuwahimiza wakenya wajitokeze kwa wingi kupewa chanjo hiyo.