Kundi la Taliban lasema limedhibiti sehemu zote za jimbo la Panjshir isipokuwa mji mkuu wa mkoa huo
2021-09-06 10:10:51| cri

Kundi la Taliban lasema limedhibiti sehemu zote za jimbo la Panjshir isipokuwa mji mkuu wa mkoa huo_fororder_VCG111344304424

Ofisa mwandamizi wa Kundi la Taliban nchini Afghanistan jana amesema, kundi hilo limedhibiti sehemu zote za jimbo la Panjshir isipokuwa Bazarak, mji mkuu wa jimbo hilo, na kwamba mapambano ya kuishambulia Bazarak yanaendelea.

Lakini kundi la National Resistance Front of Afghanistan NRF limesema kwenye mtandao wa kijamii kwamba, wanateka tena sehemu zilizokaliwa na kundi la Taliban, ambalo kundi la Taliban limepata hasara kubwa ya kifo na majeruhi kwenye mapambano.

Baada ya kundi la Taliban kudhibiti mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, tarehe 15 mwezi Agosti, Muungano wa kupinga Taliban ulianzisha kundi la NRF, ambao unaongozwa na makamu wa rais wa Afghanistan Amrullah Saleh na Ahmad Massoud, mtoto wa kiongozi wa zamani wa Muungano wa Kaskazini, Ahmad Shah Massoud.