Wapiganaji wa kundi la IS wafanya shambulizi kaskazini mwa Iraq
2021-09-06 09:14:05| CRI

Askari polisi 13 wameuawa na wengine watano kujeruhi katika mashambulizi yaliyofanywa na wapiganaji wa kundi la IS katika mkoani Kirkuk, kaskazini mwa Iraq.

Afisa Polisi wa Mkoa huo Bw. Abbas Taye amesema, wapiganaji hao walishambulia kituo cha polisi karibu na mji mkuu wa mkoa wa Kirkuk, Rashad, na kuua polisi wawili, halafu wamefanya shambulizi la mabomu dhidi ya magari mawili ya polisi na kusababisha vifo na majeruhi zaidi kwa polisi.