China yatoa salamu za pongezi kwa timu yake iliyoshiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Walemavu
2021-09-06 09:19:41| CRI

China yatoa salamu za pongezi kwa timu yake iliyoshiriki kwenye Michezo ya Olimpiki ya Walemavu_fororder_VCG31N1338171569

Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Baraza la Serikali la China zimetoa salamu za pongezi kwa timu ya China iliyoshiriki kwenye Michezo ya 16 ya Olimpiki ya Walemavu iliyofungwa Jumapili mjini Tokyo, Japan.

Katika salamu hizo, Kamati Kuu ya CPC na Baraza la Serikali zimesema, katika michezo hiyo, timu ya China ilishika nafasi ya kwanza kwa kupata medali 96 za dhahabu, 60 za fedha na 51 za shaba, matokeo yaliyoleta heshima mpya kwa taifa na watu wa China, na kuonesha maendeleo ya michezo ya walemavu nchini China.