Afrika Kusini yamruhusu rais wa zamani Zuma kupewa matibabu nje ya gereza
2021-09-06 10:50:01| cri

Habari kutoka televisheni ya taifa ya Afrika Kusini imesema Idara ya usimamizi ya magereza ya Afrika Kusini jana ilitangaza kuwa imeidhinisha rais wa zamani Jacob Zuma kupewa matibabu nje ya gereza kwa mujibu waripoti husika za matibabu.

Idara hiyo imesema hali ya sasa ya afya ya Zuma inaendana na kanuni ya kupewa matibabu nje ya gereza, ambapo kiongozi huyo wa zamani atamaliza muda wake wa kifungo uliosalia akipewa matibabu kwenye jamii, lakini lazima afuate kanuni maalum na kusimamiwa kabla ya kumaliza muda wake wa kifungo.

Serikali ya mkoa wa KwaZulu Natal imesema inawasiliana na viongozi wa juu kuhusu kumwachia huru Zuma kutokana na uzee wake akiwa na umri wa miaka takriban 80.