Maonyesho ya kutangaza bidhaa za Afrika kwa kupitia mtandao yazinduliwa
2021-09-07 08:20:12| CRI

Maonyesho ya kutangaza bidhaa za Afrika kwa kupitia mtandao yazinduliwa_fororder_791

Maonyesho ya kutangaza bidhaa za Afrika kwa kupitia mtandao wa internet na shughuli maalumu ya uuzaji wa bidhaa za Afrika kwenye mtandao moja kwa moja kupitia Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) zimezinduliwa rasmi jana hapa Beijing.

Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Afrika katika wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wu Peng amesema, China haitafuta urari wa biashara katika ushirikiano kati yake na Afrika, na inatumai kwa dhati kuongeza uagizaji wa bidhaa za Afrika na kunufaika kwa pamoja na matokeo ya maendeleo.

Bw. Wu Peng amesema, shughuli hizo zitasaidia watu wa China kununua bidhaa kutoka Afrika kwa bei nafuu zaidi, na bidhaa za Afrika hasa mazao ya kilimo kuuzwa kwa wingi nchini China kutasaidia kuongeza mapato ya wakulima wa Afrika. Pia amesema, kutangaza bidhaa za Afrika kwa kupitia mtandao wa internet nchini China kunaonyesha moyo wa kunufaishana wa ushirikiano kati ya pande hizo mbili.