Serikali ya muda ya Afghanistan kuundwa ndani ya siku kadhaa zijazo
2021-09-07 08:26:12| CRI

Serikali ya muda ya Afghanistan kuundwa ndani ya siku kadhaa zijazo_fororder_msemajitaliban

 

     Msemaji wa Taliban nchini Afghanistan Zabihullah Mujahid jana amesema, serikali ya muda ya nchi hiyo itaundwa ndani ya siku kadhaa zijazo.

Mujahid amesema serikali mpya itashirikisha pande zote, na maofisa wa kijeshi wa serikali ya zamani wataalikwa kujiunga na idara mpya ya usalama. Amesema vita nchini humo imemalizika, na ana matumaini kuwa Afghanistan itakuwa nchi yenye utulivu, na wavamizi hawawezi kuijenga upya nchi hiyo, kwani kujenga na kuendeleza Afghanistan ni majukumu ya Waafghanistan wenyewe.

Vilevile amesema, kundi la Taliban linapenda kujenga uhusiano wa utulivu pamoja na nchi jirani, pia linazitaka nchi jirani zitoe msaada katika ukarabati na maendeleo ya Afghanistan.