China yatoa wito wa kuachiwa kwa rais wa Guinea anayeshikiliwa na waasi
2021-09-07 09:04:55| CRI

China yatoa wito wa kuachiwa kwa rais wa Guinea anayeshikiliwa na waasi_fororder_timg (50)

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin amesema, China inapinga waasi nchini Guinea kuchukua madaraka kwa nguvu, na inatoa wito kwa waasi hao kumwachia huru rais wa nchi hiyo, Alpha Conde.

Wang amesema, China inafuatilia kwa karibu hali nchini Guinea, na kutaka pande zote husika zijizuie kwa kufuatia maslahi ya kimsingi ya taifa na raia, na kutatua masuala kwa njia ya mazungumzo, ili kulinda amani na utulivu nchini humo.

Habari nyingine zinasema, kiongozi wa waasi hao, Mamady Doumbouya, amekutana na waziri mkuu na mawaziri wa nchi hiyo, na kutangaza kuwa serikali ya umoja wa taifa itaundwa hivi karibuni.