Mawaziri wa G20 wakubaliana mpango wa kuzipatia nchi maskini chanjo ya COVID-19
2021-09-07 08:47:19| CRI

Mawaziri wa afya wa Kundi la Nchi 20 (G20) wamechukua hatua ya kutekeleza mpango wa kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona kwa kundi la watu walio hatarini katika nchi masikini.

Waziri wa Afya wa Italia Roberto Speranza amesema, baada ya mazungumzo ya siku mbili, mawaziri hao walikubaliana kuhusu mpango mpana wa kutoka msaada wa kifedha na chanjo ili kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi hivyo katika nchi maskini zaidi.

Katika taarifa yao ya pamoja iliyotolewa jana jumatatu, mawaziri hao wamkubaliana kuwa wanapaswa kutoa ujumbe wa nguvu wa ushirikiano, mshikamano na haki, kwa imani thabiti kuwa hakuna anayeachwa nyuma.

Kando ya mazungumzo hayo, waziri wa afya wa Ujerumani Jens Spahn amesema, nchi yake imeahidi kutoa msaada wa dozi milioni 100 za chanjo ya COVID-19 kwa nchi maskini itakapofika mwisho wa mwaka huu.