Marekani yaondoka nchini Afghanistan mikono mitupu baada ya vita ya miaka 20
2021-09-07 14:44:25| CRI

Marekani yaondoka nchini Afghanistan mikono mitupu baada ya vita ya miaka 20_fororder_VCG111345166194

Kamanda Mkuu wa jeshi la Marekani Jenerali Kenneth McKenzie tarehe 30 Agosti alitangaza kwamba Marekani imemaliza kuondoa vikosi vyake kutoka nchini Afghanistan, hali ambayo inaonesha kuwa operesheni ya kijeshi ya Marekani iliyoendelea kwa miaka 20 nchini Afghanistan imemalizika rasmi. Vita hii ambayo ilianzia kupinduliwa kwa utawala wa Taliban ilimalizika kwa Taliban kuchukua madaraka tena. Wakati huohuo Marekani pia imeshindwa kutimiza lengo lake la kuangamiza ugaidi nchini Afghanistan, badala yake, makundi ya kigaidi yamestawika kila kila mahali nchini humo.

Tarehe 11 Septemba, mwaka 2001, magaidi waliteka nyara ndege za abiria na kugonga minara miwili ya Jengo la Biashara ya Kimataifa huko New York, ambayo ni ishara ya uchumi wa Marekani, na kuwaua takriban watu 3,000. Karibu mwezi mmoja baadaye, Marekani ilianzisha vita dhidi ya Afghanistan kwa kisingizio cha “kupambana na ugaidi”. Wakati huo, Marekani ilikuwa na malengo mawili ya kimkakati: moja lilikuwa kudonoa utawala wa Taliban ili kuondoa "mwavuli wa kinga" wa kundi la kigaidi la al-Qaeda lililoongozwa na Bin Laden, na lingine lilikuwa kuifanya Afghanistan itekeleze "demokrasia" ya kimarekani. Lakini, miaka 20 baadaye, baada ya kulipa zaidi ya dola trilioni 2 za kimarekani kwa matumizi ya vita na maisha ya wanajeshi 2,461, Marekani imeshindwa kabisa kutimiza malengo hayo mwili.

Hapo awali, wakati Rais Joe Biden wa Marekani alipoelezea ni kwanini alifanya uamuzi wa kumaliza vita huko Afghanistan, alidai kwamba Marekani imepata "ushindi mzuri" nchini humo, na kwamba “jeshi la Marekani limeondoa kabisa wapiganaji wanaopinga Marekani, na hawawezi kufanya mashambulizi zaidi dhidi ya Mareknai”. Lakini, mara tu sauti yake iliposhuka, tawi la Khorasan la Kundi la Kigaidi la IS lilifanya shambulizi kubwa la kigaidi katika Uwanja wa Ndege wa Kabul tarehe 26 Agosti, kwa kulenga wanajeshi wa Marekani waliokuwa wanaondoka, na kusababisha vifo vya watu 170, wakiwemo wanajeshi 13 wa Marekani.

Marekani imepigana na magaidi nchini Afghanistan kwa miaka 20, lakini idadi ya makundi ya kigaidi nchini humo imeongezeka hadi zaidi ya 20 kutoka chini ya 10. Takwimu zinaonesha kuwa, mwaka 2001, kulikuwa na mashambulizi 20 ya kigaidi nchini Afghanistan, ambayo yalisababisha  vifo vya watu 177. Lakini mawaka jana, mashambulizi 2,373 ya kigaidi yalitokea nchini humo na kusababisha vifo vya watu 6,617. Afghanistan ime kuwa nchi ziliyokumbwa zaidi na mashambulizi ya kigaidi duniani. Vita iliyoanzishwa na Marekani na kuwepo kwa vikosi vya nchi hiyo nchini Afghanistan kwa muda mrefu vimeleta uhasama mkubwa wa wenyeji kwa Marekani, na kuchochea ukuaji wa makundi ya kigaidi. Baada ya shambulizi la Uwanja wa Ndege wa Kabul, Gazeti la New York Times la Marekani limesema, ingawa Marekani na washirika wake wamezuia makundi ya kigaidi yakiwemo IS na Al Qaeda kupata maeneo ya kujiendeleza, lakini zimeshindwa kuyazuia kuendelea kufanya mashambulizi ya kigaidi. Makundi hayo yamepata njia za kukabiliana na shinikizo kubwa la jeshi la Marekani.

Licha ya hayo, jaribio la Marekani la kukuza “demokrasia ya Kimarekani” nchini Afghanistan pia limeshindwa. Wakati jeshi la Marekani lilipoingia nchini Afghanistan, aliyekuwa Rais wa Marekani George W Bush alifuata “nadharia ya amani ya kidemokrasia”. Kwa maoni yake, utawala wa kiovu,uonevu na chuki katika Mashariki ya Kati, ni vyanzo vya matishio dhidi ya Marekani, na njia ya kutokomeza vyanzo hivyo ni “demokrasia ya Kimarekani”.

Lakini sasa miaka ishirini imepita. Vita ya Marekani nchini Afghanistan imesababisha vifo na majeruhi ya zaidi ya Waafghanistan 100,000, na zaidi ya watu milioni 10 kukimbia makazi yao. Ile inayoitwa serikali ya kidemokrasia ya Afghanistan iliyoungwa mkono na Marekani imedhoofishwa kabisa na ufisadi na uzembe. Kile Marekani inacholeta kwa watu wa Afghanistan sio amani na demokrasia, lakini ni maumivu na uchungu usio na mwisho. Balozi wa zamani wa Marekani nchini Afghanistan Peter Michael McKinley kwenye makala yake juu ya hali ya hivi karibuni nchini Afghanistan, amesema jaribio la Marekani la kuilazimisha Afghanistan kupokea mfumo wa demokrasia ya kimagharibi limeshindwa. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China Hua Chunying amesema, hali ya Afghanistan inathibitisha tena kwamba mfumo wa demokrasia uliolazimishwa kupokelewa na nchi nyingine hautadumu kwa muda mrefu.

Kuanzia Vietnam hadi Afghanistan, hali halisi imethibitisha kwamba vita haitaweza kuileta Marekani manufaa kila mara. Sasa ni wakati wa Marekani kusahihisha vitendo vyake!