Watu 30 wauawa katika shambulizi kaskazini mashariki mwa DRC
2021-09-07 08:53:02| cri

Msemaji wa jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemkorasia ya Kongo (DRC), Jul Ngongo, amethibitisha kuwa watu kadhaa wameuawa katika shambulizi lililofanywa jumamosi na watu wenye silaha katika kijiji kimoja cha mkoa wa Ituri kaskazini mashariki mwa nchi hiyo, ambalo limesababisha vifo vya watu wasiopungua 30.

Bw.Ngongo amesema kuwa shambulizi hilo lilisababisha hasara kubwa, lakini hakuweka wazi idadi ya majeruhi.

Hata hivyo, Shirika moja lisilo la kiserikali limesema, wapiganaji wa kundi la “Democratic Alliance” la Uganda ADF walishambulia kijiji hicho na maiti 30 za watu zimepatikana katika eneo la tukio.