Li Keqiang kushiriki Mkutano wa saba wa viongozi wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa (GMS)
2021-09-08 10:52:09| cri

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wang Wenbin amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa kufuatia mwaliko wa waziri mkuu wa Kambodia Hun Sen, waziri mkuu wa China Li Keqiang atashiriki kwa njia ya video kwenye mkutano wa saba wa viongozi wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Kanda Ndogo ya Greater Mekong (GMS) utakaofanyika tarehe 9 mwezi huu.

 

Wang Wenbin alisema mkutano huo una umuhimu mkubwa kwa nchi mbalimbali za kanda hiyo katika kushirikiana kukabiliana na janga la virusi vya Corona na kuhimiza ufufukaji wa uchumi. Alisema kwa muda mrefu, China imeshiriki na kuhimiza vizuri mchakato wa ushirikiano wa kiuchumi wa kanda hiyo. Inatarajiwa kuwa pande mbalimbali zitatumia mkutano huo kama fursa ya kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa maendeleo ya kikanda kwa pamoja na kuingiza nguvu mpya ya ustawi na ufufukaji kwa nchi hizo husika.