Naibu waziri mkuu wa China akutana kwa njia ya video na rais mteule wa Mkutano wa mabadiliko ya tabianchi wa UM
2021-09-08 16:16:47| Cri

Naibu waziri mkuu wa China Bw. Han Zheng amekutana kwa njia ya video na Bw. Alok Sharma, rais mteule wa Mkutano wa 26 wa mabadiliko ya tabianchi wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika huko Glasgow, Uingereza, ambaye yuko ziarani nchini China.

 

Katika mazungumzo yao, Bw. Han amesema kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kunahitaji mshikamano na ushirikiano wa dunia nzima. Akizitaka pande mbalimbali kuchukua hatua halisi kukamilisha mazungumzo kuhusu Mkataba wa Paris, na kuhakikisha usimamizi wa mambo ya hali ya hewa duniani unaendelea kwa kufuata njia ya wazi, shirikishi, na yenye maafikiano.

 

Naye Bw. Sharma ameeleza kuwa Uingereza inaipongeza China kwa juhudi zake kubwa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Pia inapenda kuimarisha mazungumzo na uratibu na China, ili kuhimiza mikutano miwili kati ya pande zilizosaini mkataba kupata matokeo mazuri.