Taliban yatangaza serikali ya muda nchini Afghanistan
2021-09-08 08:47:18| CRI

Taliban yatangaza serikali ya muda nchini Afghanistan_fororder_微信图片_20210908085019

Taliban imetangaza kuunda serikali ya muda nchini Afghanistan, na kumteua Mullah Hassan Akhund kukaimu wadhifa wa Waziri Mkuu wa nchi hiyo.

Msemaji wa kundi hilo Zabihullah Mujahid amewaambia wanahabari mjini Kabul kuwa, Mullah Abdul Ghani Baradar na Abdul Salam Hanafi wameteuliwa kukaimu nafasi ya manaibu waziri mkuu, huku Mullah Mihammad Yaqoob, ambaye ni mtoto wa mwanzilishi wa kundi la Taliban, kuwa kaimu waziri wa ulinzi. Uteuzi mwingine uliofanywa na kundi hilo ni wa waziri wa mambo ya nje, ambapo Amir Khan Muttaqi atakaimu wadhifa huo, Sarajuddin Haqqani anakuwa kaimu waziri wa mambo ya ndani, na Abas Stanikatzai ameteuliwa kukaimu nafasi ya naibu waziri wa mambo ya nje.

Mujahid amesema uteuzi wa serikali ya muda sio rasmi kwa kuwa nafasi hizo zote ni za kukaimu, na nafasi nyingine zitatangazwa katika siku zijazo.