China imetoa zaidi ya dozi bilioni 2.11 za chanjo ya COVID-19
2021-09-08 08:47:59| CRI

Kamati ya Taifa ya Afya nchini China (NHC) imesema jana kuwa, zaidi ya dozi bilioni 2.11 za chanjo ya virusi vya Corona zimetolewa nchini humo mpaka kufikia jumatatu.

Naibu mkuu wa kitengo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa katika Kamati hiyo Wu Liangyou amesema, mpaka kufikia jana jumatatu, zaidi ya watu bilioni 1.09, sawa na asilimia 77.6 ya idadi ya watu nchini China wamepata japo dozi moja ya chanjo, na zaidi ya watu milioni 967.7 wamepata chanjo kamili.

Pia amesema, karibu dozi milioni 162.3 za chanjo ya virusi vya Corona zimetolewa kwa watoto wenye umri wa kati ya miaka 12 hadi 17.