China yahimiza ushirikiano kati yake na Afrika kubadilika na kuinua kiwango
2021-09-09 08:55:35| CRI

China yahimiza ushirikiano kati yake na Afrika kubadilika na kuinua kiwango_fororder_timg (50)

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje China Bw. Wang Wenbin jana amesema, maonyesho ya kutangaza bidhaa za Afrika kwa kupitia mtandao yaliyoanza hivi karibuni, ni hatua moja ya utekelezaji wa “mpango wa wenzi mpya wa uvumbuzi wa kidijitali kati ya China na Afrika”, na yamepongezwa na kushirikisha na nchi nyingi za Afrika.

Bw. Wang amesema, hivi karibuni China na Afrika pia zilifanya shughuli mbalimbali ambazo zilifuatilia sekta za sayansi na teknolojia, uvumbuzi na uwekezaji. Amesema shughuli hizo zinazingatia kuunganisha mahitaji ya nchi za Afrika katika ushirikiano na kujiendeleza, kuhimiza ufufukaji wa uchumi barani Afrika, na kuonyesha kithabiti imani na nia ya China ya kuhimiza ushirikiano kati yake na Afrika, na kuubadilisha na kuinua kiwango chake, ili kutimimiza maendeleo yenye sifa ya juu.