Waziri wa mambo ya nje wa China ahudhuria mkutano wa kwanza wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi jirani na Afghanistan
2021-09-09 08:52:04| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China ahudhuria mkutano wa kwanza wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi jirani na Afghanistan_fororder_3bf33a87e950352a7e551baed5eeedfbb3118b92

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi jana jumatano hapa Beijing, alihudhuria mkutano wa kwanza wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi jirani na Afghanistan kwa njia ya video.

Wang Yi amesema, Afghanistan bado inakabiliwa na changamoto kubwa, ikiwemo masuala ya kibinadamu, maisha ya watu na janga la virusi vya Corona, na kwamba nchi jirani zinataka kuisaidia nchi hiyo kuondokana na vurugu. Ameongeza kuwa nchi hizo jirani zinapaswa kuwa na athari nzuri katika maendeleo ya Afghanistan katika msingi wa kuheshimu uhuru wa mamlaka ya nchi hiyo na ukamilifu wa ardhi yake.

Amesema China imeamua kutoa msaada wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 30.96 kwa Afghanistan, unaojumuisha nafaka, vifaa vya kujikinga wakati wa msimu wa baridi, chanjo na dawa.