Reli ya SGR yanufaisha eneo la Afrika Mashariki na Afrika nzima kwa ujumla
2021-09-09 14:08:33| CRI

Reli ya SGR yanufaisha eneo la Afrika Mashariki na Afrika nzima kwa ujumla_fororder_SGR

Ni jumapili nyingine tunapokutana msikilizaji katika kipindi hiki cha Daraja kinachokujia kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing. Baadhi ya mambo niliyokuandalia katika kipindi cha leo ni ripoti inayohusu reli ya SGR ya nchini Kenya ambayo imeleta faida kubwa kwa Afrika Mashariki na bara zima kwa ujumla, lakini pia tutakuwa na mahojiano kuhusu awamu ya pili ya mradi wa Televisheni za satelaiti uliozinduliwa wa kampuni ya husuma za televisheni ya StarTimes ya China.