Udhalilishaji wa kijinsia na rushwa ya ngono kazini vyaleta madhara makubwa kwa wanawake
2021-09-09 14:22:08| Cri

Udhalilishaji wa kijinsia na rushwa ya ngono kazini vyaleta madhara makubwa kwa wanawake

Vitendo mbalimbali vibaya dhidi ya mwanamke vimekuwa vikimuathiri moja kwa moja na kumfanya kuwa dhalili katika jamii. Wanawake wamekuwa wahanga wa matukio mengi tu makubwa ya udhalilishaji wa kingono iwe majumbani, maofisini au hata kutakiwa rushwa ya ngono pale wanapoomba kazi au kuomba chuo pia na kama akitaka kufaulu kuna baadhi ya maprofesa na walimu humtaka mwanamke huyu kingono. Katika kipindi cha leo tutaangalia vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia pamoja na rushwa ya ngono kazini.