ECOWAS yaamua kusitisha uanachama wa Guinea
2021-09-09 11:51:07| cri

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS jana Jumatano iliitisha mkutano maalumu wa mtandaoni kujadili hali ya kisiasa nchini Mali na Guinea, ambapo washiriki walipitisha uamuzi wa kusitisha uanachama wa Guinea, wakiitaka nchi hiyo kurejesha utaratibu wa kikatiba na kumuachia huru mara moja rais Alpha Condé wa nchi hiyo.

Mkutano huo pia umekubali kutuma ujumbe wa ngazi ya juu kwenda Guinea ili kufanya usuluhishi. Lakini mkutano huo haukutangaza vikwazo vyovyote vya kiuchumi dhidi ya Guinea.