Rais wa China ahudhuria mkutano wa nchi za BRICS
2021-09-09 21:25:23| CRI

Rais wa China ahudhuria mkutano wa nchi za BRICS_fororder_1127846045_16312045587031n

Rais Xi Jinping wa China amehudhuria mkutano wa 13 wa viongozi wa nchi za BRICS ambazo ni Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini kwa njia ya video.

Kwenye mkutano huo, rais Xi ametangaza kuwa China itatoa msaada zaidi wa dozi milioni 100 za chanjo ya COVID-19 kwa nchi zinazoendelea. Amesema hadi sasa China imetoa dozi bilioni moja za chanjo hiyo kwa nchi nyingine duniani, na itatoa dozi bilioni moja nyingine hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu. 

Amesema, China pamoja na nchi nyingine za kundi hilo zitakuza ushirikiano wao katika sekta mbalimbali kwa pande zote, na kuanzisha uhusiano wa kiwenzi wa karibu na uhalisia zaidi, ili kukabiliana na changamoto na kuanzisha mustakabali mzuri kwa pamoja.

Rais Xi amesema, huu ni mwaka wa 15 tangu kuanzishwa kwa kundi la BRICS, na katika kipindi hicho, nchi hizo zimeshikilia kufungua mlango, kusikilizana na kutendeana kwa usawa, kuhimiza mawasiliano ya kimkakati na uaminifu wa kisiasa, kuheshimu mifumo ya kijamii na njia ya maendeleo, na kuendelea kutafuta njia sahihi ya kuishi pamoja kati ya nchi tofauti. Amesema ushirikiano wa BRICS utadumu kwa mafanikio bila kujali changamoto zilizopo.