Kenya yatangaza ukame kuwa janga la kitaifa
2021-09-09 08:56:19| cri

 

 

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta jana ametangaza kuwa ukame, uliokumba maeneo mengi nchini humo, kuwa ni janga la kitaifa.

Rais Kenyatta ameagiza mashirika husika kuongoza juhudi za serikali ili kuzisaidia familia zilizoathiriwa, ikiwa ni pamoja na usambazaji wa maji na msaada wa chakula.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Kenya imesema, uamuzi huo unafuatia mkutano kati ya rais na viongozi 85 kutoka Maeneo Kame (ASAL).

Taarifa hiyo pia imesema, maelezo zaidi ya hatua za serikali za kupunguza ukame zitatolewa kwa wakati unaofaa.