Ushirikiano kati ya China na Marekani kwenye sekta zenye utoaji mdogo wa hewa ya ukaa watajwa kuwa ni nyanja muhimu ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili
2021-09-09 11:50:45| cri

Naibu waziri wa biashara wa China Wang Shouwen amesema, China na Marekani kufanya ushirikiano kwenye sekta zenye utoaji mdogo wa gesi ya ukaa, si kama tu ni njia yenye ufanisi kwa nchi hizi mbili kutimiza malengo yao ya kupunguza utoaji wa hewa ya kaboni, bali pia ni nyanja muhimu ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani.

Bw. Wang amesema hayo kwenye kongamano la ushirikiano kwenye sekta zenye utoaji mdogo wa hewa ya ukaa kati ya mikoa na majimbo ya China na Marekani, lililofanyika kando ya Mkutano wa 21 wa Uwekezaji na Biashara wa Kimataifa wa China. Amesema mageuzi yanayoendelea nchini China ya kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa pamoja na soko lake kubwa la ndani vitatoa fursa nyingi za maendeleo kwa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani. Inakadiriwa kuwa, ifikapo mwaka 2030, mapato ya sekta zenye utoaji mdogo wa hewa ya ukaa nchini China yatafikia Yuan trilioni 23, ikiwa ni sawa na dola za kimarekani trilioni 3.56.