CMG na IOC zasaini mkataba mpya kuhusu hakimiliki za ubunifu za Michezo ya Olimpiki
2021-09-09 22:00:50| CRI

CMG na IOC zasaini mkataba mpya kuhusu hakimiliki za ubunifu za Michezo ya Olimpiki_fororder_1

Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa IOC leo zimetangaza kwa pamoja kuwa, zimeanzisha ushirikiano wa kutangaza Michezo ya Olimpiki katika China bara na Macau katika kipindi kipya, ikiwa ni pamoja na Michezo ya 25 ya Olimpiki ya Majira ya Baridi itakayofanyika ya miji ya Milan na Cortina d’Ampezzo, Italia, Michezo ya 34 ya Olimpiki ya Majira ya Joto itakayofanyika mwaka 2028 huko Los Angeles, Michezo ya 26 ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya mwaka 2030 na Michezo ya 35 ya Olimpiki ya Majira ya Joto itakayofanyika huko Brisbane .

CMG na IOC zasaini mkataba mpya kuhusu hakimiliki za ubunifu za Michezo ya Olimpiki_fororder_2

Siku hiyo mkurugenzi mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong na mwenyekiti wa IOC Bw. Thomas Bach wamesaini mkataba huo kupitia mtandao wa Internet.