Serikali na wasomi wa nchi nyingi wapinga kufanya utafutaji wa chanzo cha COVID-19 kuwa suala la kisiasa
2021-09-09 11:52:31| cri

Hivi karibuni, Idara ya ujasusi ya Marekani ilitunga ripoti ya uchunguzi kuhusu chanzo cha COVID-19. Serikali, wasomi na wataalamu wa nchi nyingi wametoa taarifa kwa nyakati tofauti kupinga kulifanya suala hilo kuwa la kisiasa.

Wizara ya mambo ya nje ya Sri Lanka imetoa taarifa kuhusu suala la chanzo cha COVID-19 ikipinga kulifanya suala hilo kuwa la kisiasa, huku ikitaka kuheshimu ripoti ya utafiti wa pamoja wa Shirika la Afya Duniani WHO.

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Bolivia ametoa taarifa kupitia mtandao wa kijamii akisema, utafutaji wa chanzo cha COVID-19 ni suala muhimu linalohusiana na binadamu wote, ambalo pia ni suala la kimsingi linalohusiana na mapambano dhidi ya COVID-19 duniani, hivyo linatakiwa kutatuliwa kwa njia ya kisayansi.

Mzinduzi wa Kituo cha uangalizi wa maendeleo ambacho ni jopo la washauri bingwa la Uganda ametoa makala ikikosoa Marekani kufanya utafutaji wa chanzo cha COVID-19 kuwa suala la kisiasa.