Watu 87 wauawa katika mapigano kati ya jeshi la Yemen na kundi la Houthi
2021-09-09 09:35:49| cri

Watu 87 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika saa 48 zilizopita katika mapambano kati ya jeshi la Yemen na kundi la Houthi nchini humo.

Afisa mmoja wa serikali ya Yemen ambaye hakupenda kutajwa jina amesema, katika saa 48 zilizopita, kundi la Houthi lilishambulia sehemu ya magharibi mwa jimbo la Marib. Ameongeza kuwa, jeshi la serikali ya Yemen lilipambana na kundi hilo kwa kushirikiana na jeshi la anga la muungano wa kimataifa unaoongozwa na Saudi Arabia.