Wizara ya Mambo ya Nje ya China: Kundi haramu linalojiita “Mahakama Maalumu ya Wauygur” kamwe halitafanikisha njama yake
2021-09-10 11:52:09| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema, bila kujali kuwa Kundi linalojiita “Mahakama Maalumu ya Wauygur” litafanya mikutano mingapi linaloita “ya kusikiliza kesi”, haitabadilisha ukweli kwamba kundi hilo ni haramu, na kamwe halitafanikisha njama yake.

Msemaji huyo amesema, mfadhili mkuu wa kundi hilo ni jumuiya ya kuipinga China World Uyghur Congress (WUC), na wale wanaojiita “wataalamu”, “majaji”, na “mashuhuda” wa kundi hilo wote wana historia mbaya ya kusema uongo na kupotosha ukweli, ambao tayari wamekuwa vichekesho kwenye jamii ya kimataifa.

Bw. Zhao Lijian amesisitiza kuwa bila kujali watacheza mchezo gani, mkoa wa Xinjiang utazidi kupiga hatua siku hadi siku, na sauti za jamii ya kimataifa za kutaka Xinjiang iangaliwe kwa haki zitasikika na kuongezeka zaidi siku hadi siku.