Uwekezaji wa China barani Afrika wazidi dola za kimarekani bilioni 47
2021-09-10 08:34:21| CRI

Uwekezaji wa China barani Afrika wazidi dola za kimarekani bilioni 47_fororder_timg (2)

Uwekezaji wa China barani Afrika umeongezeka kutoka dola milioni 210 za kimarekani mpaka kufikia dola bilioni 47 za kimarekani tangu kuanzishwa kwa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mwaka 2000.

Hayo yamo kwenye ripoti iliyotolewa jana na Kitengo cha Uchumi na Biashara ya Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Shanghai. Kutokana na tathmini iliyofanywa katika nchi 54 za Afrika kwenye upande wa ukubwa wa kiuchumi, mfumo wa kiviwanda, nguvu ya uwekezaji, matishio, mazingira na fursa za uwekezaji, ripoti hiyo imeeleza sababu kuu zinazozingatiwa katika uwekezaji barani Afrika, na pia mwelekeo wa siku zijazo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kampuni za China zimetoa mchango mkubwa katika mageuzi ya kiviwanda, utulivu wa kijamii na ustawi wa kiuchumi barani Afrika kwa kuboresha uhamishaji wa teknolojia, kuimarisha ugavi katika maeneo husika, na kutoa fursa za ajira.

Ripoti hiyo imeonyesha kuwa, mpaka kufikia mwaka 2019, China ilikuwa imewekeza katika nchi 52 kati ya 54 barani Afrika.