Marekani yadhalilishwa kwa kuharibu uhusiano kati ya China na Afrika
2021-09-10 14:50:17| cri

 图片默认标题_fororder_VCG111338665681

Kwa muda mrefu, baadhi ya wanasiasa nchini Marekani wamefanya kila wawezalo kuchafua jina la China kwa kuisema kama ni hatari na kufanya ukoloni mambo leo ili kuharibu uhusiano kati ya China na Afrika. Hata mkuu wa Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani (AFRICOM) Jenerali Stephen Townsend aliliambia Shirika la Habari la Marekani AP kuwa “China inatafuta mahali pa kuhifadhi silaha na kuzifanyia matengenezo meli za kivita barani Afrika…"

 

Hata hivyo kauli hizi za uchochezi zimekosolewa na mkurugenzi wa Mpango wa Utafiti wa China na Afrika katika Shule ya Mafunzo ya Juu katika Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, Marekani Bibi Deborah Brautigam. Alisema kwenye gazeti la The Washington Post kuwa “maelezo mengi yaliyotolewa na wanasiasa wetu (wa Marekani) kuhusu China si sahihi”. Ameongeza kuwa shughuli za kiuchumi za China barani Afrika hazina asili ya kunyonya, bali “zinalingana na maslahi ya kiuchumi ya nchi hizi za Afrika, kutoa nafasi za ajira kwa watu na kuboresha miundombinu.”

 

Akitoa mfano wa kilimo, Bibi Brautigam alisema kwenye kitabu chake maarufu cha “Kama Afrika itailisha China?” kuwa “mada kuhusu China ikiwa wawekezaji ‘inapora maslahi’ barani Afrika zimetajwa katika makala nyingi kwenye mtandao wa internet, ambazo zinatisha na kujaa siri, lakini kinachoshangaza watu ni kuwa kati yao ripoti za utafiti ni chache sana.” Amegundua katika utafiti wake kuwa katika ardhi ya China yenye eneo la hekta milioni 6 inayosemekana kununuliwa na China, ni hekta laki 2.5 tu zilinunuliwa kihalisia. Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa limegundua kwenye utafiti wake wa mwaka 2021 kuwa kampuni za China barani Afrika zinafanya juhudi kushiriki kwenye sekta ya kilimo kwa uwajibikaji.

 

Katika miaka ya hivi karibuni, pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” lilitoa nafasi za maendeleo kwa nchi za Afrika, haswa katika ukanda wa Afrika Mashariki, imetoa misaada mingi kwa ujenzi wa miundombinu mikubwa kama vile bandari na reli za kisasa. Wakati Marekani inaichukulia kama ni tishio, viongozi wa nchi za Afrika wanaona ni matokeo ya ushirikiano mzuri. Kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika mjini Beijing mwaka 2018, rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alitoa hotuba akisema, “tukiwa nchi au bara, tunatamani kujenga uhusiano imara wa kiwenzi na China.” Naye naibu waziri wa fedha na mpango wa maendeleo wa Liberia Augustus Flomo alisema, “China ni mwenzi wetu muhimu wa ushirikiano wa kimkakati.”

 

Kwa mujibu wa ripoti ya uwekezaji wa kampuni za China barani Afrika iliyotolewa mwishoni mwa mwezi uliopita na Baraza la Biashara kati ya China na Afrika, katika miongo miwili iliyopita tangu FOCAC izinduliwe, uwekezaji wa moja kwa moja wa China barani Afrika umeongezeka kwa wastani wa asilimia 25 kwa mwaka. Katika kipindi cha janga la virusi vya Corona, uwekezaji wa China barani Afrika uliongezeka kutoka dola za kimarekani bilioni 2.71 za mwaka 2019 hadi dola za kimarekani bilioni 2.96 za mwaka 2020. Katika sekta ya biashara, katika miongo miwili iliyopita, thamani ya biashara kati ya China na Afrika iliongezeka mara 20 na kufikia dola za kimarekani bilioni 187 mwaka 2020.

 

Tofauti na China, tangu mwaka 2020, uwekezaji wa Marekani barani Afrika ulipungua kwa miaka mfululizo. Wakati huohuo, thamani ya biashara kati ya Marekani na Afrika pia ilipungua kutoka dola za kimarekani bilioni 141.9 za mwaka 20087 hadi dola za kimarekani bilioni 46 za mwaka 2020. Tofauti na jinsi China na Afrika zinavyoshirikiana katika sekta ya uchumi na biashara, kwa miaka mingi Marekani inajizatiti kwenye sekta ya jeshi. Kamandi ya jeshi la Marekani barani Afrika AFRICOM imekuwa ikijiingiza kijeshi katika nchi 50 za Afrika na wakati mwingine kuingilia kijeshi mara kwa mara kwenye mambo ya siasa ya nchi, mwaka 2011 vita ya Libya, mwaka 2012, 2020, 2021 nchini Mali, mwaka 2013 Misri, mwaka 2015 Burkina Faso. Kwa mujibu wa tovuti ya Msaada kwa Nje ya Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Marekani, mwaka 2017 Marekani ilitoa msaada wa dola za kimarekani bilioni 7.5 kwa nchi 11 za Afrika zilizopokea msaada wa Marekani kwa wingi zaidi, na kati ya fedha hizo, dola 1.5 zilikwenda kwa sekta ya jeshi. Ni wazi kuwa Marekani iliacha kuendeleza uhusiano wa kibiashara na nchi za Afrika, na baada ya kuona maendeleo ya uhusiano wa kibiashara kati ya China na Afrika yanaimarika, Marekani inaona ni China “imeiba keki” yake na kuanza kutoa shutuma zisizo na msingi ili kuchafua jina la China.

 

Uwazi na ujumuishi ni kiini cha uhusiano kati ya China na Afrika. Mwezi Mei mwaka 2021, mjumbe wa baraza la taifa la China na waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi alitangaza kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini New York kuwa China itaanzisha “pendekezo la kuunga mkono Afrika kuendeleza uhusiano wa kiwenzi”, ikishirikiana na nchi za Afrika na Umoja wa Afrika ili kutoa motisha zaidi kwa Afrika kujitafutia maendeleo endelevu. Pendekezo hilo limesisitiza kuwa Afrika ni jukwaa la ushirikiano wa kimataifa, na si uwanja wa mashindano kwa nchi kubwa. “pendekezo hilo linashikilia utaratibu wa pande nyingi, na kuwa wazi kwa nchi na mashirika yote ya kimataifa … katika msingi wa kanuni ya “Afrika kuongoza, usawa na uwazi.”

 

Kamwe China hailengi kuchukua nafasi ya Marekani, wala kuanzisha mfumo sambamba wa uchumi wa kimataifa ili kushindana na mfumo wa kiuchumi unaoongozwa na Marekani. Katika miongo kadhaa iliyopita, China imekuwa mnufaika mkuu wa utandawazi, na inapenda kuendelea kuhimiza mfumo huo wa kimataifa wa uwazi na utandawazi. Mapendekezo ya ushirikiano kama vile “Ukanda Mmoja, Njia Moja” sio tu yanaweza kuinua ubora wa maisha ya watu wa Afrika, bali pia ni sehemu muhimu ya mlolongo wa uzalishaji duniani, na kutoa mchango kwa juhudi za kupunguza umaskini na kukuza uchumi duniani. Juhudi hizo zinastahiki kutajwa kuwa chanya, na wala si tishio.