Rais Xi atuma salamu za heri kwa walimu
2021-09-11 18:12:27| cri

 

Rais Xi Jinping wa China ametuma salamu za heri kwa walimu kote nchini China kabla ya Siku ya Walimu ya China ambayo ilikuwa Ijumaa.

Kwenye salamu zake Rais Xi ametoa wito kwa walimu kutoa mwongozo mzuri kwa wanafunzi.  

Rais Xi amesema hayo akijibu barua kwa wawakilishi wa vitengo vya kufundisha vilivyopewa jina la mwana jiofizikia wa China Huang Danian, profesa katika Chuo Kikuu cha Jilin. Bw. Huang aliisaidia China kufanya maendeleo katika uchunguzi wa kina wa ardhi.

Amesema mwalimu bora anapaswa kuwa mtu mwenye maarifa makubwa ya kuchangia na mwadilifu, na kuwataka walimu wote katika vyuo vikuu kote China, kuendelea kukuza utu, kuzingatia kufundisha na kuendelea kuwa wabunifu.

Rais Xi amesema walimu wanatoa mwongozo mzuri kwa wanafunzi na kuwalea kuwa vijana wenye uwezo wenye maadili na busara, na kuendelea kufundisha na kufanya uvumbuzi.