China yatoa waraka wa mwongozo wa kuimarisha mageuzi juu ya mfumo wa fidia ya uhifadhi wa mazingira ya kiikolojia
2021-09-13 09:23:38| cri

Serikali ya China imetoa waraka wa mwongozo wa kuimarisha mageuzi juu ya mfumo wa fidia ya uhifadhi wa mazingira ya kiikolojia, ambao umeeleza kwa kina hatua za China katika kutimiza malengo ya fidia ya kiikolojia ya muda mrefu kwa mwaka 2025 na mwaka 2035.

Mwongozo huo umesema hadi kufikia mwaka 2025, China inapaswa kumaliza kimsingi kutunga mfumo wa fidia ya kiikolojia unaoendana na maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na kuanzisha mfumo wa fidia wenye hadhi ya soko na aina tofauti, na jamii nzima itashiriki zaidi kwenye shughuli za kuhifadhi mazingira ya kiikolojia. Na hadi kufikia mwaka 2035, China itakuwa na mfumo wa fidia ya kiikolojia utakaokidhi mahitaji ya ustaarabu wa kiikolojia katika zama mpya.