China yaitaka Japan iangalie kwa usahihi historia yake ya uvamizi
2021-09-14 09:11:50| cri

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian jana aliitaka Japan iangalie kwa usahihi historia yake ya uvamizi, na kuchukua hatua za kiutendaji ili kuweza kuaminiwa na nchi jirani za Asia na jumuiya ya kimataifa.

Akizungumzia suala la “wanawake wa kuwastarehesha wanaume”, Zhao amesema kuwalazimisha wanawake wawastarehesha wanaume ni uhalifu mkubwa dhidi ya ubinadamu uliofanywa na nguvu za kijeshi za Japan, hii imekuwa hali halisi ya kihistoria yenye ushahidi. Kitendo cha Japan cha kuidhinisha kubadilisha historia hiyo kwenye vitabu vya kiada kimekwepa wajibu wa kihistoria na kukanusha historia yake ya uvamizi, ambacho kitakataliwa na watu wote wanaopenda amani. Japan inapaswa kuangalia kwa usahihi historia yake ya uvamizi, na kutatua suala la “wanawake wa kuwastarehesha wanaume” kwa njia mwafaka yenye msimamo wa uwajibikaji na ukweli.