Mwakilishi wa China katika UM aunga mkono mchakato wa Ethiopia wa kutafuta amani na maendeleo
2021-09-14 09:14:25| cri

Mwakilishi wa China katika UM aunga mkono mchakato wa Ethiopia wa kutafuta amani na maendeleo_fororder_埃塞 头图

Balozi wa China katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Jiang Duan amesisitiza kuwa China inaunga mkono juhudi za Ethiopia za kulinda mamlaka na umoja wa nchi, ikizitaka pande zote zinazohusika kuondoa mikwaruzano na tofauti, na kupunguza hali ya wasiwasi kwa njia ya kisiasa, ili kuweka mazingira kwa ajili ya kutafuta maafikiano ya amani.

Balozi Jiang amesema hayo wakati alipohutubia Mkutano wa 48 kuhusu suala la haki za binadamu nchini Ethiopia kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.

Balozi Jiang pia ameeleza kuwa China inatumai jamii ya kimataifa itaunga mkono serikali ya Ethiopia kusimamisha vita kwa pande zote, kuhimiza mchakato wa kutafuta maafikiano ya kitaifa, na kupinga nguvu za nje kuingilia mambo ya ndani ya Ethiopia kwa kisingizio cha haki za binadamu.